Sunday, October 24, 2010

Tambua mpenzi anaye kudanganya/anakulaghai.

Mpenzi wako anakosa maamuzi binafsi. Hii haimaaanishi kwamba atakwenda nje kutafuta mpenzi mwingine, lakini mtu asiye na uhuru fulani katika mawazo yake mara nyingi huwa akitafuta msaada sehemu nyingine. Kama mahitaji ya mtu huyu hayatatimizwa, basi hutafuta sehemu nyingine kwa mtu mwingine ili kutimiza hisia zake.

Kila mara mpenzi wako anamlaumu mtu Fulani. Anajaribu kukufanya ufikirie kwamba aina ya watu kama hao hawamvutii kabisa, ingawa kwa hakika ndani ya nafsi yake hubakia mvuto wa siri kwa mtu wa aina hiyo. Zaidi ya yote mpenzi wako anaanza kulaumu vitu kadhaa kuhusu wewe ambavyo awali aliona vina mvutia na kumtamanisha.

Mpenzi wako anaanza tabia ya kujifungia ndani mnapokuwa pamoja, wakati hapo awali alizoea, kuuacha mlango wazi. Kwa mfano hataki muoge pamoja kama zamani, anapobadili nguo anataka usimtazame na mambo mengine kadha wa kadha.

Mpenzi wako hujiona kama mkosefu wakati unapomfanyia kitu fulani kizuri. Wewe unaonekana kuwa mtu unayefanya maisha yake kwamba mabaya na uhusiano kama kitanzi.

Kwa kufanya kitu kizuri unamlazimisha mwongo huyu kufikiria kuhusu usaliti anaokufanyia.

Mpenzi wako anaonyesha hamu ya kusoma kitabu zaidi au kuangalia televisheni kuliko kuzungumza na wewe au kufanya mapenzi na wewe.

Mpenzi wako kwa muda mrefu amekuwa mwenye mawazo lakini kila unapomuuliza hataki mjadili kuhusu mambo yake binafsi.

Mpenzi wako anaonyesha kushtuka anapoamshwa. Hali hii husababishwa na kutokuwa na uhakika ni chumba gani alicholala na yuko katika kitanda cha mpenzi gani kati ya wawili alionao.

Tabia ya mpenzi wako inawafanya rafiki zako kuanza kukuuliza nini kinachoendelea. Rafiki wa karibu na ndugu wa familia watabaini hali ya kutokuwepo na amani baina yenu wawili kabla nyie hamjaelewa sawasawa.

Tabia ya kulala kwake itabadilika, kama alikuwa akichelewa kulala, sasa anaweza kuwahi kwa kisingizio kwamba amechoka.

Anaweza kuwa kweli amechoka, lakini tabia hiyo inapoendelea ujue kuna jambo, kwani mara nyingine huwa hapendi hata kuzungumza mnapokuwa kitandani, tofauti na zamani.

No comments:

Post a Comment