Wednesday, May 3, 2017

Hatua za kumchagua Mchumba

Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.
Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

1. Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

2. Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

3. Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

4. Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

5. Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

6. Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

7. Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

8. Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

9. Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

10. Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.

Saturday, September 17, 2016

ANZISHA MAHUSIANO MAPYA WAKATI MOYO WAKO HAUNA DOWA LOLOTE

Si lazima uwe kwenye uhusiano muda wote, ukiona mambo hayajakaa vizuri usiyalazimishe.

Kabla haujaanza uhusiano mwingine, ebu JIULIZE ni kitu gani umejifunza Katika uhusiano wako uliopita.

Kuna msemo usemao KUJUA chanzo cha tatizo ni Nusu ya KUTATUA Tatizo, Je umefahamu tatizo lilofanya uhusiano wako wa 1, 2 na 3 kuvunjika? Ulishawahi kukaa chini kujiuliza? Ulipata majibu gani?

Usiingie kwenye uhusiano mpya kabla haujapona MAJERAHA ya uhusiano uliopita, Kujipa muda kuwa peke yako ni TIBA tosha.

Usiingie kwenye uhusiano mpya ili kumkomoa X wako, Isije ukajikomoa mwenyewe.

Usiingie kwenye uhusiano mpya ili kupoza moyo wako isije ukawa unazidisha Kidonda,

Usiingie kwenye uhusiano mpya ili kuondoa upweke, isije ukauzidisha huo upweke.

Usiingie kwenye uhusiano mpya ukitegemea kumpata mtu BORA kuliko X wako, isije ukawa unaruka Mkojo, unakanyaga.........?

Usiwe kama Nyani kuruka-ruka kwenye miti, mara tawi hili, mara tawi lile. Lakin pamoja na uhodari wote wa Nyani wa kuruka kwenye miti lakini kama siku ya KUFA imefika, miti yote HUTELEZA.

SI LAZIMA MUDA WOTE UWE KWENYE UHUSIANO, JIPE MUDA KUWA PEKE YAKO, CHUKUA LIKIZO YA MAPENZI.

"MOYO ULIOJERUHIWA, HUJERUHI, MOYO ULIOPENDWA HUPENDA "

Sunday, November 8, 2015

NAMNA YA KUACHA KUJICHUA AU KUPIGA PUNYETO

Karibuni tena wapendwa wasomaji wa blog hii ya MAHUSIANO kama kawaida leo tena unapata shule nyingine ambayo namatumaini inaendelea kukujenga kiakili na Kimahusiano

Makala iliyopita niliongelea maana na madhara yanayosababishwa na kupiga punyeto nilipokea simu nyingi ambazo zilitaka pia niongelee suluhisho au jinsi gani mtu anaweza kuacha punyeto kabisa

Punyeto kama tulivyoongea ni tatizo la tabia na linaweza kudhibitika kabisa kama matatizo mengine yeyote.

FANYA YAFUATAYO....

Acha kuangalia video za ponograph: video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

Epuka kukaa nyumbani peke yako; mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa, kuumwa kichwa na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.
acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema ivoivo, kama unaacha acha mara moja.

Tafuta mpenzi kama huna kabisa: ukiwa na mpenzi madhara ya punyeto kama kupungukiwa nguvu za kiume yatakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto. pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.

Anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine:hii itakufanya ue bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko, pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala

Uzoefu unaonyesha, mtu anayepiga punyeto, hata kama ameathiriwa na tatizo la punyeto kwa kiwango gani, endapo atafanikiwa kutopiga punyeto kwa muda wa siku arobaini mfululizo, mtu huyo hatopiga tena punyeto katika siku zote za maisha yake kwani tayari mtu huyo atakuwa amerudia katika hali yake ya kuto kuwa addicted tena na upigaji punyeto, na atalichukia kabisa hata jina la tendo hilo achilia mbali tendo lenyewe.

MAELEZO ZAIDI........

Pia ileleweke kuwa Sio rahisi kwa mtu aliyekuwa addicted na punyeto kustahimili kujizuia kupiga punyeto kwa muda wa siku arobaini mfululizo. Anaweza kujizuia kupiga punyeto kwa siku mbili lakini baada ya hapo ataendelea tena na mchezo wako.



JARIBU PIA DAWA HII....



PILIPILI

Pilipili inayo hitajika hapa ni yoyote ile ili mradi iwe kali sana, ( Ila inayo pendekezwa ni pilipili mbuzi ama pilipili kichaa, pilipili hoho haihusiki hapa ).


MATUMIZI


Kwanza kabla ya kujua matumizi ni vyema ukatambua muda ambao huwa unapiga punyeto ( Mara nyingi huwa ni asubuhi baada ya kuamka,wakati wa kuoga ama usiku kabla ya kulala ).

Chukua pilipili zako, zipasulie kwenye viganja vya vidole vyako na kujipakaza katika viganja vya vidole vyako. Unaweza kutumia pili moja kwa kila kiganja, na kwa kila muda ambao huwa unapiga punyeto lakini unaruhusiwa kujipakaza zaidi ya pilipili moja.

Ukishajipaka pilipili kwenye viganja vya vidole vyako, moja kwa moja unakuwa umekwisha jilazimisha kutokufanya punyeto, kwa sababu ukipiga punyeto kwa viganja ambavyo vina pilipili utawashwa sana wala hautaweza kufurahia tendo hilo.


JAMBO LA KUZINGATIA : Hakikisha unakuwa na walau pilipili mbili mpaka nne kila unapokuwa katika maeneo ambayo yanaweza kukuchochea kufanya punyeto.


UFANISI WA DAWA HII : Dawa hii inawafaa wale tu ambao wamedhamiria kutoka mioyoni mwao kuacha kufanya punyeto. Kwa wale ambao hawajadhamiria haitaweza kuwasaidia.



MWISHO,TUNAWATAKIA KILA LA HERI WATU WOTE WATAKAO AMUA KUJARIBU KUTUMIA NJIA HIZI ILI KUACHANA NA SUALA LA UPIGAJI PUNYETO. NITAFURAHI SANA ENDAPO MTATUPA FEEDBACK/MREJESHO BAADA YA HIZO SIKU AROBAINI TANGU MUANZE KUFANYA ZOEZI HILI. MUNGU AWAPE NGUVU NA AWABARIKI.

Friday, September 5, 2014

KUBEMENDA MTOTO: HAKUNA UKWELI WOWOTE ULE JUU YA SUALA HILI BALI USAFI NDIYO UNAHITAJIKA WAKATI WA KULEA MTOTO

KUNA hili suala linaloitwa 'kubemenda' mtoto, watu wanadai kuwa sperms huwa zinaleta madhara kwenye maziwa ya mama na kumdhoofisha mtoto kiafya na wengine wanasema ukimshika mtoto baada ya sex pia ina madhara.

kiukweli suala la Kubemenda ni imani potofu (myth) na hakuna uhusiano wa sperms na maziwa ya mama katika kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa kushirikiana tendo la ndoa au kumshika mtoto baada ya sex.

Je, nini maana ya kubemenda mtoto?
Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba kubemenda mtoto ni pale wanandoa wanapojihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya kujifungua) kwa maana kwamba sperms huharibu maziwa ambayo mtoto ananyonya, si kweli hakuna uhusiano wowote kati ya maziwa ya mama na sperms katika kuathiri afya ya mtoto. Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na mke kushika mimba miezi mwili tu au mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea) na huitwa ni mtoto ambaye amebemendwa, kitu ambacho ni imani potofu kwani kuna wanandoa wengi tu wamezaa watoto waliopishana mwaka na wote wana afya njema kabisa.

Tatu kubemenda ni kitendo cha mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa (sex) na akirudi ndani huendelea na tendo la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu hakuna kitu kama hicho.

Jambo la msingi ni kufuata ushauri wa kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya kujifungua.

Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii imani potofu
Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa mwingine baada ya mwaka au hata kutoka nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa kama suala la usafi na lishe bora litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.

Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani kama hiyo kwa wanandoa? Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu. Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.

Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?

Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea.

Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya sex au muda wowote. Ni jukumu la baba na mama wa mtoto kuhakikisha wanatumia muda wao kuhakikisha mtoto anapata lishe bora na mahitaji yote ya msingi ya mtoto ili kukua na kuwa na afya njema na si kujinyima kujihusisha na tendo la ndoa wakihofia mtoto kuonekana amebemendwa.

Pia suala la usafi wa mazingira ya mtoto anapoishi (vyombo vya kutumia kwa chakula cha mtoto, usafi wa mwili wa mtoto na mama na baba pia) ni muhimu sana kwani baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa mume na mke kuhakikisha wanakuwa safi tena bila kujihusisha na kumnyonyesha mtoto huku hawajanawa au kuoga.


MUHIMU
Suala la kubemenda (binafsi naweza kuita ni utapiamlo au kwashakoo kingereza- Kwashiorkor) huzungumzwa sana na jamii za “mtanzania wa kawaida” huwezi kusikia katika nchi zilizoendelea na watu ambao wameenda shule na wanafuata misingi ya afya na uzazi katika kulea watoto wao na pia mke na mume kuwa karibu kimapenzi.

Dhana hii hauwezi kuisikia katika nchi zilizoendelea ndiyo maana nasema kuwa hii ni dhana potofu tuu!!!!

Wednesday, August 27, 2014

Things Every Woman Does That Destroy A Relationship

Women are not the only ones who can destroys a relationship, but there are a few things that a lot of women do that send men running for the hills. In a every successful relationship, both parties can talk about what is bothering them or common problems that can be avoided.
If you’re starting feel a rift between you and your guy, you can easily bring him back into the fold by making a few changes to yourself and the way that you handle issues when they come up.
Here are 5 things that women do to ruin a relationship.

1. Too Much Nagging.
Nagging can be one of the most annoying things to a man.
Women that nag instantly get eye rolls from their spouses. It doesn’t matter if it’s over the trash, dirty dishes or laundry, nagging your guy to do something over and over again is going to get on his nerves.
Keep in mind that an overbearing mother during childhood can affect a man well into the rest of his life. If you nag and he has had this in his past, he could find it so annoying that he leaves you. If he’s doing something that really bothers you, be a mature adult and talk to him about it. Let him know what he’s doing and how much it bothers you. Once he knows that it’s a problem, he will change his ways.

2. Insisting On Marriage Very Early.
Marriage is one of those things that every woman wants.
There isn’t a girl on this earth that doesn’t want to walk down the aisle with the guy of her dreams. But when you’re pushing marriage too soon you’re going to ruin what you have. Marriage is a huge step and it should not be taken lightly.
Properly planning for a future with a guy is not something that can happen overnight. If you’ve been with your guy for over a year and he’s not event talking about marriage you might have a problem on your hands. But if you’ve been together for a couple of months and you’re trying to get a ring, you need to slow it down.
Remember that a marriage is a marriage, not just the wedding.

3. Wanting Him To Do Everything.
Here’s a very big problem that a lot of women face.
Traditionally, men have been the breadwinner in relationships. However, the last 20-30 years have made women even more successful than men in the workplace. Some women talk about equality until it’s time for the check. If you’re going to be in a relationship, you need to meet him halfway. This doesn’t just extend to finances though. Compromise is the foundation for every relationship and without it you will have a very unhappy man.
Always getting your way or always letting him get his way is not going to accomplish anything. Make sure that your relationship is a 50/50 partnership or you will find your guy leaving you.

4. Not Saying What Bothers Them.
One of the things that makes men crazy is when a girl does not talk about what is bothering them.
Men like strong women that aren’t afraid to tell them what they want and what they don’t want. So many women clam up and get distant when they don’t like something about the relationship. If you don’t talk to your guy he could just give up all together and leave you.

The truth is that men love when there are no problems in a relationship. When you work through your problems he’s going to feel closer to you. Men are used to women getting distant when they don’t like something or when they are angry so when you open up to him, you will find that he is much more open and respectful.
Don’t let things fester. This will only make it worse for you and him.

5. Threatening You Want To Quit.
This is something that all men hate in a relationship.
If you are threatening to leave him, you better be ready to do it. When your guy does something that you can’t stand and you threaten to leave him, he sees this as a bluff. It’s not until you actually leave him that he’s going to respect you.
So many women threaten to leave their guys every day and never do. The guy sees this as an empty threat and the behavior just recycles over and over again. This can easily ruin the relationship.

Men that get away with things and never have ramifications are going to walk all over you. Make a decision and actually leave him if the behavior does not get corrected.

Sunday, October 13, 2013

SABABU ZA KUKAUKA KWA UKE WA MWANAMKE WAKATI WA KUFANYA MAPENZI......

Swala la kukauka kwa uke mara baada ya mwanake kufika kileleni ni la kwaida kwa wanawake wengi na huwa na sababu mbali mbali ambazo mimi nitakutajia kwa kifupi tu kama ifuatavyo:-

1-Mwanamke huitaji kunyegeshwa tena baada ya bao la lake la kwanza, inategemea lilipopatikana kama kwenye Kipele G, Kwenye Kisimi, Mwisho wa Uke au kuta za uke. Ikiwa amepata bao "via" kisimi hapo lazima atahiji muda kidogo wa kupumzika kama dakika kumi 5+ kisha wewe mpenzi wake ni wajibu wako kumnyegesha tena kwa kucheza na sehemu nyngine za mwili wake mbali na Kisimi. Inaweza kuwa kum-busu, kumla denda huku unamshika-mshika na kadhalika

2-Mwanamke kuwa na uwezo mdogo wa kungonoana (low sex drive/libido) ni wazi kuwa hamjuani hivyo yawezekana yeye yuko hivyo na mara baada ya wewe kupiga bao la kwanza ksiha kurudi na "kumpigisha" yeye bao lake ndio ilikuwa mwisho wa "game" mpaka kesho au labda wiki ijayo kama sio mwezi mwezi ujao. Kama ulihitaji tena kwenda basi ulitakiwa kumfaya aendelee kuwa "interested" kiakili nakimazingira zaidi ya kimwili na pia ungepaswa kutumia kilainisho kwa ajili ya Condom au hata K-Y Jel.

3-Mwanamke kutokuvutiwa na ufanyaji wako, kama ulivyosema kuwa ilikubidi uache nje-ndani, swala l a kungonoana ni pana na sio kusimamisha kisha kupiga nje-ndani mwanzo mpaka mwisho Kuna wanawake kibao baada ya kibaruti cha kwanza inabidi uanze upya kuwatuliza a.k.a kuwa NYEGELESHA. Dawa yake kwa wengi usikazanie NJe ndani Nje ndani sana kama ushambarutisha tayari. Cheza sindimba au msondongoma katika mduara bila kuvuta filimbi nje wakati unaASALISHA mambo mengine!Baada yamuda kadhaa wakati unahisi au unasikia pumzi fulani ndio endeleza pupa kama navyohisi unafanya.Hii hasa kama unacheza mkao wa kimishenari ).

4-Mwanamke kutokuwa na mapenzi pia inaweza kuwa sababu ya Uke wake kuwa mkavu mara baada ya zile nyege mshindo kumalizika/kumtoka (baada ya yeye kufikia Mshindo), mwanamke kama hana mapenzi huishiwa hamu ya kuendelea kungonoka haraka sana mara tu baada ya bao lake la kwanza.

5-Kuchoka au Uvivu, mwanamke kama kachoka au mvivu hali hiyo ya ukavu ukeni hujitokeza kwa vile akili yake inakuwa haipo/haizingatii kilekinachofanyika bali saa ngapi atapata nafasi ya kwenda kulala/pumzika. Condom huwa hazisababishi Uke kukauka tena japokuwa inashauriwa kubadili au kutumia kilainisho kilichotengenezwa kwa ajili hiyo. Makampuni mengi ya bidhaa hzi yanatoa mafuta maalum kabisa kwa ajili ya kukuongezea ile hali ya ulaini amabo unakulinda wewe kwa kuzuia Condom kupasuka/chanikakutokana na ukavu wa Uke na vilevile kumuongezea mwanamke raha ya tendo.

Condoms hazimsababishii mwanamke maumivu bali ile hali ya wewe kumfanya mwanamke mwenye uke mkavu kwa muda mrefu ndio inasababisha maumivu.Ili ufurahie Ngono basi ni vema ukatafuta mwanamke mmoja umpendae na yeye akupende na mfanye tendo kwa ushirikiana na kumbuka ku-focus kwenye kufurahia tendo zaidi kuliko kupiga mabao na mambo yatakuwa bomba kabisa.

Friday, May 18, 2012

Sababu za Vijana Kujingiza katika Tabia za Hatari na Namna ya Kuwasaidia

Katika makala hii tunashirikisha namna ya kuwasaidia vijana ili waweze kuvuka vikwazo vinavyoweza kuwafanya wasifikie malengo waliojiwekea maishani mwao. Tunatambua kwamba, yapo mambo mengi yanayoweza kuwachelewesha au kuwakwaza vijana kutofikia malengo yao ya maisha.

Baadhi yake ni kama:

Dawa za kulevya Ulevi VVU/Ukimwi Mimba kabla ya wakati, n.k. Katika makala hii, tunaelezea sababu chache zinazopelekea vijana (wasichana) kupata mimba kabla ya wakati. Pia tunapendekeza namna ya kuweza kuwasaidia ili wasijikute katika mtego huu na pia waweze kufikia malengo yao katika maisha yao. Ingawa sababu hizi zinawalenga wasichana moja kwa moja, hata hivyo zinaweza kutumika kwa wavulana pia, kwa vile wavulana wanajiingiza katika mambo haya kirahisi kuliko wasichana. Bi. Tricia M. Davis amefanya utafiti kati ya wasichana wapatao 500 wenye umri wa miaka chini ya 19, waliowahi kupata mimba zaidi ya mara moja. Katika utafiti wake anaeleza sababu saba zilizojitokeza na kuchangia katika hawa kupata mimba zaidi ya mara moja. Katika makala yake, “An Examination of Repeat Pregnancies Using Problem Behaviour Theory”, iliyochapishwa katika Jarida la Journal of Youth Studies (Vol. 5,no.3, 2002, pp.337-351), anafafanua kwa kina juu ya tatizo hili. Hivyo tunaamini kuwa baada ya kupitia maelezo haya, kama walezi wa vijana tutakuwa na upana wa mawazo na kuwawezesha vijana namna ya kupanga malengo mazuri katika maisha yao na jinsi watakavyoweza kuyafikia malengo hayo.

1. Kutokuwa na Malengo ya Maisha Sababu ya kwanza, kati ya saba zilizoorodheshwa ni kutokuwa na malengo maalum katika maisha. Vijana wenye malengo endelevu katika maisha huwa wanachelewesha tendo la ndoa na hivyo kutopata mimba kabla ya wakati. Kijana anapokuwa amejiwekea malengo makubwa katika maisha yake, hakika atakuwa makini zaidi na daima atajiepusha na tabia zinazoweza kumpelekea kutofikia malengo yake. Kwa mfano, ikiwa kijana fulani aliye katika kidato cha kwanza (Form I) na ana lengo la kuwa rubani wa ndege au kiongozi mashuhuri katika nchi au mtu yeyote maarufu, ni wazi atajishugulisha zaidi na mambo ya masomo. Hali hii haina maana kwamba hatajihusisha na starehe zinazoambatana na ujana! La hasha. Ila hata kama anakwenda disko basi atatambua lengo lake na atajua dosari inayoweza kumpata endapo atajilegeza na kufuata vishawishi vya ndani ya disko. Kwake atatambua kirahisi kuwa akifanya ngono anaweza kupata mimba na hivyo kushindwa kufikia malengo yake. Msichana mwenye lengo kuu kama hili ni tofauti na yule asiyekuwa na malengo. Msichana asiyejua la kufanya baada ya kumalizia shule ya msingi ni rahisi kwake kujiingiza katika tabia za hatari. Hali halisi ya vijana wengi wa Afrika Mashariki ni kuwa hawana uhakika na maisha baada ya shule ya msingi. Kwa hiyo, sisi ambao tunahusika na malezi ya vijana tutambue kwamba njia rahisi ya kuwawezesha vijana kutokupata mimba, wala kujiingiza katika tabia za hatari, haitoshi kuwaambia “muwe wazuri”, bali kuhakikisha kuwa wanaweka malengo makuu katika maisha yao.

2. Kutojithamini ya Kutosha Hii ni hali ya kijana kujiona hafai kwa chochote katika familia anamotoka au katika jamii ya watu inayomzunguka. Hisia hii inampelekea kujichukia na kupata msukumo wa kutaka kutafuta thamani ya nafsi yake kirahisi. Njia mojawapo ya kufanya hivi ni kujaribu mambo ya mapenzi. Kwa msichana wa hali hii ni rahisi kufikiri thamani yake inatokana na tendo hili la ngono kwani linaambatana na lugha nzuri wanazotumia wavulana na ahadi au zawadi anazoweza kupewa. Wasichana wanaotoka katika familia zisizo na upendo wa kweli kati ya wazazi (baba na mama) ni rahisi kudanganyika na kutafuta thamani zao nje ya familia. Au mzazi hasa baba, anayetumia lugha ya ukali daima au lugha ya mfumo dume humfanya binti kutojisikia wa thamani. Na hali ile ya kupendwa inapokosekana nyumbani, basi ni wazi msichana huyu anapokutana na mvulana mwenye maneno matamu anaweza kudanganyika kirahisi. Pia misamiati kama, “kulizaliwa kwa bahati mbaya” na nyingineyo inaweza kupelekea kwa binti kutojipenda. Ikumbukwe kwamba nyumbani ni shule ya kwanza ambapo kila mmoja wetu anajifunza maana ya utu na namna ya kupenda na kupendwa na wengine. Kwa upande wa msichana, baba ndiye mwanamume wa kwanza anayetokea kuhusiana naye, hivyo ana jukumu la kujenga thamani ya huyu binti anayekua. Hivyo ni dhahiri kwamba kama tunapenda kuwasaidia vijana kutokupata mimba kabla ya wakati, ni bora kuhakikisha kama kijana fulani anathamini utu wake. Tunaweza kuwasaidia vijana kwa kuandaa semina zinazohusu kujitambua na kuwasaidia kuanza safari ya kutafakari, “Mimi ni nani?,” na “Thamani yangu inatokana na nini?” Hii itawasaidia kutambua kwamba thamani ya mtu haitegemei watu wengine wala wanavyosema, hata si umbo alilo nalo, bali ni hali ya ndani. Thamani ya mtu ipo ndani ya utu wake, yaani nafsini mwa mtu mwenyewe.

3. Kutowajibika Sababu nyingine inayoweza kumpelekea kijana kupata mimba kirahisi ni kutokuwa na tabia za kuwajibika (External locus of control). Kutowajibika kuna maana ya mtu anavyoeleza matukio mbalimbali ya maisha yake na jinsi gani anavyojiepusha na tukio lile. Tabia hizi zaweza kuonekana hata katika mambo madogo madogo. Kwa mfano, kijana akidondosha kitu fulani na kusema, “Kitu hiki kimedondoka”, yeye anajaribu kutafsiri tukio lile kuwa hakuhusika nalo kabisa. Au mwingine anapovunja glasi na kusema, “Glasi imevunjika” anajaribu kutowajibika na tukio hilo. Sote tunatambua jinsi Adamu alivyotaka kujiepusha na kutokuwajibika kwa kosa alilofanya katika bustani ya Edeni. Mungu alipomuuliza, “Umefanya nini?” Adamu alimjibu Mungu, “Mwanamke uliyenipa ndiye alinidanganya nami nikala…” Adamu hakutaka kuwajibika na tendo lake. Hali kadhalika kijana mwenye mazoea ya kutowajibika katika mambo madogo madogo, ni rahisi kwake kujiingiza katika ngono na hatimaye kupata mimba bila kujali au kuwajibika. Wasichana wenye tabia ya kusema, “Shetani alinidanganya” au “Tulikuwa tunajaribu,” wanaonyesha dalili za kutowajibika na tendo walilofanya. Ni dhahiri kwamba msichana wa namna hii hajajifunza kutokana na kosa la mwanzo, hivyo ni rahisi kwake kurudia kitendo hicho hicho. Sisi kama walezi wa vijana tunahitaji kuanza kuwazoesha vijana tulio nao kuwajibika katika mambo madogo madogo. Kupendekeza kwa wazazi, walezi, na vijana wenyewe kwa kuwapa nafasi za kujaribu shughuli zinazoendana na umri wao, na hasa katika kumiliki vitu vyenye thamani ndogo. Hii itawafanya kujisikia kuwa wenye kuchukua hatamu ya maisha yao.

4. Ukosefu wa Uchaji Ukosefu wa uchaji ni ile hali ya kijana kutojali mambo ya kiimani. Vijana wanaokuwa na hali hii ya kutojali mambo ya kidini na imani kwa ujumla wanajiweka katika mazingira rahisi zaidi ya kujiingiza katika tabia za hatari. Hii ni kwa sababu wanakuwa wamezamisha dhamiri zao zisiwasumbue wanapokuwa wamekosea. Kwa upande mwingine, vijana wanaojihusisha na vikundi mbalimbali vya kukuza imani, wanapata malezi mazuri juu ya dhamiri zao na hivyo hata kama wakikosa ni rahisi kwao kurudi katika msingi mzuri wa maadili. Vikundi hivi ni kama vile vya kutafakari Neno la Mungu, fokolare, vikundi vya kiutume na vinginevyo. Uchaji hapa si kuja kanisani Jumapili kama sheria fulani, bali ni ile hali ya kuguswa na Mungu; kuwa na mang’amuzi binafsi ya upendo wa Mungu. Uchaji hapa si tendo la kurudia rudia sala fulani, bali ni hali ya kutafakari na kujiweka katika hali ya kuunganika na Mungu. Vijana wenye mazoea haya wanajenga polepole ndani yao uwezo wa kuchunguza dhamiri na kutathmini siku ilivyokuwa kabla ya kulala (Examination of coscience). Hata katika sala binafsi wanaweza kugundua kosa dogo walilolifanya katikati ya siku bila wao kujua kwa sababu ya mahangaiko ya maisha. Hali ya namna hii inaweza kutumika kama kinga kwa makosa makubwa kama tabia za hatari tunazozizungumzia katika makala hii. Hivyo, kuna umuhimu mkubwa wa kupendekeza mpango fulani utakaohakikisha vijana wanapata fursa ya kujituliza na kutafakari maisha yao ya kiroho. Katika matoleo ya Mlezi yaliyopita, tumewahi kuzungumzia juu ya maisha ya kiroho kwa vijana. Tunaweza kurejea na kuona namna gani tunaweza kuwa na mpango utakaowasaidia kuanza safari hii ya kuwa na uchaji.

5. Mazingira Duni ya Nyumbani Hii ni sababu nyingine inayoweza kuwapelekea vijana kujiingiza katika tabia za hatari. Kama msichana anaishi na mzazi mmoja, kuna uwezekano wa binti kupata mimba mapema kutokana na kuathiriwa na mfano wa muundo wa familia anayoishi. Pia kwa wale wanaotoka katika familia ambazo mume na mke si waaminifu, kuna uwezekano mkubwa wa kijana kushawishika na kuanza mambo ya mapenzi mapema. Hata hivyo, vijana wanahitaji kusaidiwa namna ya kuzipokea familia zao, na kuamini kuwa si lazima waige mfano potovu wa wazazi wao. Zaidi ya hayo, ni kutambua kwamba kuna mambo wanayoweza kuyabadili na mengine wanahitaji kukubali nayo. Ni lazima vijana wajue hawawezi kutawala tabia za wazazi wao ila wanaweza kukabili tabia zao wenyewe. Kwa kufanya hivyo wanakuwa mashujaa wa mazingira magumu waliyojikuta nayo.

6. Mshinikizo wa Rika Mshinikizo wa rika unaweza kuwalazimisha vijana lakini si kwa sehemu kubwa! Vijana wanaweza kushawishika kufanya ngono au kujiingiza katika tabia za hatari kutokana na hadithi zinazosimuliwa na wenzao. Kila mmoja hujidai kuwa alijaribu mambo haya na kuelezea jinsi alivyojisikia. Hali hii inaweza kuchochea hamu ya kutaka kujaribu mambo yale ya hatari. Kama kijana tayari ana malengo na anajithamini si rahisi sana kupeperushwa na upepo huu wa masimulizi haya. Lakini kama kijana hana malengo maalum katika maisha na hajui thamani yake, basi ni wazi mshinikizo wa rika una nafasi kubwa ya kumpotosha.

7. Tabia ya Kupenda kujaribu mambo mapya Vijana wenye tabia ya kupenda kujaribujaribu ili kujua ladha yake hata bila kujali madhara yake wanaweza kuingia katika mtego kirahisi. Kwa kufikiri kuwa wanaweza kujaribu tendo lolote la hatari mara moja tu na kuacha, kumbe kunaweza kuwa mtego wa kudumu. Hata mara moja inaweza kuwa mara nyingi. Kuna methali ya Kiswahili inayosema, ‘Mwonja asali haachi kuchonga mzinga.’ Vijana wanatakiwa kueleweshwa kuwa kila tabia inaanza kwa tendo moja la awali.

Hitimisho Sababu zilizotolewa hapa juu zinaweza kutumika kama kinga ya kuwasaidia vijana kutojiingiza katika tabia za hatari – kama vile utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi, na kupata mimba kabla ya wakati. Basi, vijana wasaidiwe kuwa na… Malengo ya maisha Hali ya kujithamini Tabia ya kuwajibika Uchaji Uwezo wa kutokuzamisha na mazingira duni ya nyumbani Msimamo wa kutofuata mkumbo, na Uvumilvu wa kutoanza tendo lisiloendana na hali ya maisha.