Sunday, October 24, 2010

Tambua mpenzi anaye kudanganya/anakulaghai.

Mpenzi wako anakosa maamuzi binafsi. Hii haimaaanishi kwamba atakwenda nje kutafuta mpenzi mwingine, lakini mtu asiye na uhuru fulani katika mawazo yake mara nyingi huwa akitafuta msaada sehemu nyingine. Kama mahitaji ya mtu huyu hayatatimizwa, basi hutafuta sehemu nyingine kwa mtu mwingine ili kutimiza hisia zake.

Kila mara mpenzi wako anamlaumu mtu Fulani. Anajaribu kukufanya ufikirie kwamba aina ya watu kama hao hawamvutii kabisa, ingawa kwa hakika ndani ya nafsi yake hubakia mvuto wa siri kwa mtu wa aina hiyo. Zaidi ya yote mpenzi wako anaanza kulaumu vitu kadhaa kuhusu wewe ambavyo awali aliona vina mvutia na kumtamanisha.

Mpenzi wako anaanza tabia ya kujifungia ndani mnapokuwa pamoja, wakati hapo awali alizoea, kuuacha mlango wazi. Kwa mfano hataki muoge pamoja kama zamani, anapobadili nguo anataka usimtazame na mambo mengine kadha wa kadha.

Mpenzi wako hujiona kama mkosefu wakati unapomfanyia kitu fulani kizuri. Wewe unaonekana kuwa mtu unayefanya maisha yake kwamba mabaya na uhusiano kama kitanzi.

Kwa kufanya kitu kizuri unamlazimisha mwongo huyu kufikiria kuhusu usaliti anaokufanyia.

Mpenzi wako anaonyesha hamu ya kusoma kitabu zaidi au kuangalia televisheni kuliko kuzungumza na wewe au kufanya mapenzi na wewe.

Mpenzi wako kwa muda mrefu amekuwa mwenye mawazo lakini kila unapomuuliza hataki mjadili kuhusu mambo yake binafsi.

Mpenzi wako anaonyesha kushtuka anapoamshwa. Hali hii husababishwa na kutokuwa na uhakika ni chumba gani alicholala na yuko katika kitanda cha mpenzi gani kati ya wawili alionao.

Tabia ya mpenzi wako inawafanya rafiki zako kuanza kukuuliza nini kinachoendelea. Rafiki wa karibu na ndugu wa familia watabaini hali ya kutokuwepo na amani baina yenu wawili kabla nyie hamjaelewa sawasawa.

Tabia ya kulala kwake itabadilika, kama alikuwa akichelewa kulala, sasa anaweza kuwahi kwa kisingizio kwamba amechoka.

Anaweza kuwa kweli amechoka, lakini tabia hiyo inapoendelea ujue kuna jambo, kwani mara nyingine huwa hapendi hata kuzungumza mnapokuwa kitandani, tofauti na zamani.

Jinsi ya kupata Mpenzi wa Kweli.

Katika mahusiano yoyote yale mtu/wewe ungependa kutambua ni kwajinsi gani mpenzi wako hakudanganyi. Sasa maswali yako unaweza kujibiwa kwa kusoma mambo yafuatayo;-

Usiipe nafasi hofu Nyote mnapaswa kuwa na hisia zenye afya ili kujenga uhusiano wenye mafanikio. Kwa mfano, siyo dalili nzuri kama unakuwa kwenye uhusiano kwa sababu tu unahofu kuwa mpweke.

Ni vibaya pia kwa mwanaume wako kusema anaupenda mchezo fulani kama anavyokupenda! Au ukiwa na msongo wa mawazo, usinase kwenye mtego wa mapenzi kwa kudhani unaweza kuwa tiba. Ni vizuri zaidi kutafuta mwanaume ambaye hahitaji utabibu.

Chunga mwendo wako
Jihadhari na chunga mwenendo wako kwani wanaume huwa makini na hushangazwa zaidi wakati wapenzi wao wanapokuwa wanafanya mambo ya ajabu. Unapozungumza naye muangalie usoni siyo sakafuni.

Usimuulize maswali mengi kuhusu kazi yake, ingawa ni muhimu kujua anafanya kazi gani, kwani anaweza kuwa jambazi ati! Anaweza kudhani unataka kumchuna tu.

Kama utashindwa kuchunga tabia yako, usishangae kama kukutana kwenu siku ya kwanza kunakuwa ndio mwisho wenu na usipojiangalia utajikuta tayari umemfunulia!

Kufanana huleta mafanikio
Hii haimaanishi unapaswa kuolewa na ndugu au mzazi wako, la hasha! Lakini unapoanza uhusiano na mtu, hakikisha unamfahamu kwanza kwa undani na jiulize mara mbili kama kuna vitu ambavyo mnalingana.
Fikiria kuhusu uhangaikaji wake katika maisha (hata kama hana uwezo mkubwa kifedha, je, anajuhudi za kuzisaka hizo fedha ama la?), ujuzi na hata mapenzi ya dhati.

Na fikiria sana kama malengo katika maisha yenu yanarandana. Nyote mnapaswa kukubaliana kuhusu athari pia za ndoa na kukabiliana nazo kama kuwa na watoto, kuishi kwenye nyumba ya mbavu za mbwa au hekalu.

Vipo vitu unavyoweza kuvitambua kwa kukutana kwenu mara moja au mara mbili, na nyote mnapaswa kuwa wazi.

Toa upinzani
Mfanyie kila uwezalo mpenzi wako ili atambue kwamba unampenda, lakini usitake kuchukulia dalili zake za kuridhika na wewe mapema ndizo zikupumbaze na kumganda.

Hapa sizungumziii kanuni – usisite kuijibu simu yake atakapokupigia au kwenda kukutana naye atakapokuita, hata hivyo, epuka kukutana naye sehemu ya uficho kama chumbani, lakini usijenge maisha yako kumzunguka yeye na wala usimlazimishe akakuelezea hisia zake.

Hakikisha kwamba yeye ni nyongeza katika maisha yako na siyo muhimili wa maisha yako.

Usiwe domokaya
Najua wengi wenu mna mambo mengi ambayo mnaweza kuyazungumza, lakini yahifadhi mengine kwa ajili ya siku nyingine. Wanaume hupenda kusikia habari mpya kila mnapokutana.

Wanawake wanapaswa kufikiria kuhusu hadithi mbili au tatu kali ambazo wanaweza kuzungumza wanapokuwa kwenye miadi, lakini wasivuke mpaka na kuanza kuzungumza mambo yanayowahusu wenyewe!

Usinune
Wanaume wengi huwa wanalalamika kwamba hupata wakati mgumu zaidi wanapokuwa na wapenzi wao, hasa katika siku ya kwanza ambapo hushindwa hata kuwabusu, kama huyo uliyenaye ndiye chaguo lako, basi usiwe mgumu, tabasamu na kama atakubusu usikwepeshe uso wako.

Karibuni katika ukurasa mpya na wa aina yake!!!

Ndugu zangu napenda kuwakaribisha katika ukurasa huu wa mahusiano. Ninaposema mahusiano namaanisha mahusiano yetu sisi kama vijana, wazee, wapenzi, marafiki, wanajamii na kadhalika.

Unakaribishwa kutoa mawazo yako, maoni au ushauri wowote kuhusu mahusiano. Toa mtazamo wako kuhusu mahusiano ili tuweze kujifunza kupitia wewe.

Naanza kwa kukuuliza swali/maswali
1. Mahusiano nini?
2. Ili mahusiano yako ya KIMAPENZI yawezekudumu utatumia mbinu gani?
3. Kwanini mahusiano mengi ya KIMAPENZI yanadumu kwa kitambo kidogo na kuvunjika?