Sunday, August 21, 2011

PUNYETO: FAIDA NA MADHARA YAKE

Punyeto

Ni nini?

Kufanya au kupiga punyeto, ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi.

Kwa hivyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono, kwani haimshirikishi mtu mwengine.

Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbali mbali za kujitomosa na kujipa papasa ya kujistarehesha.

Hakuna mtu anayezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama.

Na, kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyengine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako, ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe.

Shughulika zaidi na sehemu ambazo zinasisimka kwa urahisi.

Unaweza kufikia kilele cha starehe yako kwa kuitomasa tomasa mboo au kisimi, lakini kutakupa hamu kubwa na ashiki, na kufikia kutoshelezwa vya kutosha, kama utapapasa pia sehemu nyenginezo za mwili wako.

KWA NINI PUNYETO HUONEKANA KUWA MAKOSA?

Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa, jambo lisilokubalika kabisa.

Lakini wanasanyansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu, ni imani za kibinafsi na chaguo la mtu.

Wanaume wengi na wanawake hupiga punyeto maishani mwao, kwa sababu huwafanya wakajisikia vizuri na huondoa dhiki za mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwengine.

Pia hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya HIV ni kichocheo tosha kinachopelekea baadhi ya watu kupiga punyeto.

FAIDA ZA KUPIGA PUNYETO.
1)Kuujua mwili wako na kujiamini zaidi linapokuja swala la kungonoka(fanya mapenzi)

2)Kuongezeka kwa hamu ya kufanya mapenzi kwa vile utakuwa unajua utamu wake.

3)Kujua "vipele vyako viliko".

4)Kutokuusaulisha mwili wako ikiwa uko nje ya uhusiano au umeamua kuwa single kwa muda.

5)Kuepuka mimba na maambukizo ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine.

Hizi ni baadhi tu ya faida zipo faida nyingi.

Pamoja na faida hizo vivle tukiangalia upande mwingine wa shilingi tunayaona haya hapa chini.

MADHARA YA KUPIGA PUNYETO.

Ifahamike kuwa kuna watu wengi sana wanatumia mikono yao kujisaga katika sehemu nyeti, Jambo hili linamadhara makubwa sana kwa binaadamu, Jambo hili kwa lugha ya kiingereza wanaliita Masturbution, ni kitendo cha mwanaume kujisugua tupu zake.



Licha ya tafsiri ya punyeto kuwalenga wanaume zaidi lakini katika mada yangu ya pili nitaelezea Usagaji na madhara yake kwani hili linahusu wanawake na hili la usagaji linaingizwa na punyeto kwani madhara yake yanakaribiana lakini tofauti inakuja jinsi ya kujirizisha.



Wanaume wengi sana wanatumia mikono mikavu kujisaga, jambo hili huwafanya waharibu mishipa ya fahamu inayounganisha uume na mfumo uliopo kwenye ubongo.



Uharibifu huu humfanya mwanaume apoteze msisimko wa kujamiiana au hata akiupata humfanya ashidwe kufikisha hisia zake kisawasawa khasa akikutana na mwenza wake ambaye sehemu zake nyeti ni laini sana tofauti na mikono alozoea kujichua nayo.



Jambo jingine hatari linalo mkabili mpiga Punyeto ni upotevu wa hisia wakati wa kujichua kwa mfano ili afike kwenye kilele lazima akuze hisia zake kwa kiwango cha juu, pengine kupita ukweli halisi ataokutana nao pindi atakapokuwa na mwanamke faraghani.



Mpiga Punyeto hajitoshelezi mpaka amlete kwenye hisia mrembo kama Miss World kisha amvike utundu wa kimahaba ampe manjonjo hadi mwenyewe atosheke, kwa namna hii mwanaume mwenye kufanya mazoea ya kufanya hisia za wanawake warembo ambao hawezi kuwapata kwa hali halisi anapokutana na kina Mwafulani wa mtaani tena sio mtundu kimapenzi, hapo kamwe hawezi kusisimka mwili na hivyo kujikuta Uume wake husimama kwa kiwango cha chini sana.



Madhara mengine yanayopatikana ndani ya kitendo hiki ni kuumwana sana na kichwa, mgongo, kupoteza nguvu za mwili na macho, madhara mengine makubwa khasa mwanamme anaejichua mara mbili au tatu kwa siku ni kushidwa kuzalisha, hii inatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume kwenye mfuko wa uzazi.



Hii yote madhara ya hapa duniani lakini kwa Mungu ni mwisho wa hisabu kwani ''Amelaaniwa mtumiaji mkono kwa kujisugua uume wake(Punyeto)


Kujichua kwa kutumia sanamu a.k.a Dildos kunaweza sababisha kusamburuka kwa nyama za nyeti zako(inategemea na aina ya sanamu), kupoteza hisia za uume halisi kutokana na kuzoea "dubwana" hizo, kifo kutokana na "shock" ikiwa unatumia ya umeme, vilevile saratani ikiwa unatumia vilainishio ili kurahisisha "dubwana a.k.a toy a.k.a Dildo" kuingia.


kujichua kupita kiasi kunaweza kusababisha kupoteza hisia uume halisi.


Friday, January 21, 2011

SABABU KUMI ZINAZOPELEKEA MAHUSIANO YA KIMAPENZI KUVUNJIKA

MIGOGORO ni jambo la kawaida katika uhusiano wa kimapenzi au ndoa. Na ndiyo maana hata kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi au ndoa si jambo la kushangaza katika jamii. Mahusiano hayavunjiki hivi hivi, zipo sababu.

Ukizifahamu sababu za kuvunjika kwa mahusiano, kama wewe ni mwathirika wa kuvunjika kwa uhusiano utapona haraka na kujifunza kupenda tena. Kwako wewe ambaye uhusiano wako na mwenzako haujavunjika, au labda hata hujawahi kuingia katika uhusiano, unapozifahamu sababu za kuvunjika kwa uhusiano itakusaidia kufahamu jinsi ya kuenenda unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi au hata ndoa, kwa mustakabali mwema
wa uhusiano wako na mwenzako.

Kati ya shughuli nzito ambazo huwakumba watu walio katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa ni kuhakikisha kuwa mahusiano yao yanakuwa imara. Ni shughuli yenye changamoto nyingi kwani huhitaji uwiano, maana mwanamume na mwanamke wameumbwa tofauti na kila mmoja ana matakwa na matarajio yake.

Sababu za kuvunjika kwa uhusiano zinaweza kuwapo nyingi na kutofautiana kutoka uhusiano huu na ule, lakini zipo kumi ambazo zinaweza kuchukuliwa kuwa kuu. Ukizifahamu utajua jinsi ya kuboresha uhusiano wako wa sasa au baadaye, au kukuweka sawa kisaikolojia kwa ajili ya uhusiano mpya.

Sababu zenyewe ni hizi zifuatazo: -

1. KUKOSEKANA KWA UAMINIFU

Kushindwa kutimiza ahadi, kusema uwongo au kufanya usaliti wa kimapenzi ni mambo
ambayo humwondolea mtu uaminifu kwa mwenzake. Kwa hakika, kukosekana kwa uaminifu ni sababu kuu ya kuyumba na hata kuvunjika kwa mahusiano yaliyo mengi.

Iwapo kuaminiana kwa msingi kabisa katika uhusiano kutavunjwa mara kwa mara, hasira za mpenzi kwa mwenzake zitalimbikizwa na hamu ya wapenzi/wenza kuendelea kuishi pamoja itapungua. Wapenzi walio katika uhusiano wenye mizizi na afya njema wanaweza kukubaliana kumaliza tofauti zao na kusonga mbele. Kama wataheshimu ahadi na viapo vyao vipya mambo yataendelea.

Kumdanganya mpenzi mara kwa mara, kumsaliti mara kwa mara na kuvunja ahadi zako mara kwa mara huufanya uhusiano kudhoofika na hatimaye nguzo yake muhimu – yaani kuaminiana – kuanguka. Hapo ndipo uhusiano hufika kikomo.

2. KUTOKUWEPO KWA UWIANO WA MADARAKA

Katika zama hizi ambapo wanawake wamezifahamu haki zao, kutokuwepo kwa uwiano mzuri katika kutoa maamuzi inaweza kuwa sababu mojawapo ya kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi au hata ndoa.

Inapotokea kuwa mmoja tu ndiye anayetoa maamuzi kuhusiana na shughuli mbalimbali, uchaguzi wa marafiki, masuala ya kifedha, masuala ya nyumbani, likizo na kadhalika, mwingine anaweza kujiona kama vile hana nafasi katika ushirika huu, hivyo kuamua kujitoa.

Katika zama hizi, wanawake wengi wanafundishwa kuwa na hisia za usawa. Iwapo itatokea mmoja wa wanandoa au wapenzi akajihisi kuwa ametengwa katika maamuzi ya msingi yakiwamo yale yanayohusiana na mustakabali wa maisha yake, ni rahisi sana uhusiano kufika kikomo.

3. KUSHIKILIA IMANI POTOFU

Katika jamii kuna imani potofu mbalimbali kuhusiana na wanawake na wanaume.
Mathalani, kuna imani kuwa wanaume ndio hupenda sana ngono kuliko wanawake au kwamba wanawake ni watu wa kusikiliza na kupelekeshwa tu.

Iwapo mmoja wa wanandoa au wapenzi ataamini katika mojawapo ya imani hizi potofu zenye msingi wa mfumo dume, au imani nyingine zozote, kuna uwezekano mtu huyu akajenga matarajio yasiyokuwa halisi – jambo ambalo hujenga uwezekano mkubwa wa kushindwa kwa uhusiano. Hapa pia kitachotakiwa ni uwiano wa nguvu kutoka pande mbili na kuepuka kuamini katika imani potofu.

4. KUMTENGA MTU NA WATU WAKE

Mojawapo ya sababu kuu za kuachana kwa wapenzi ni mmoja kujihisi ametengwa na
marafiki zake aliotoka nao mbali, ndugu, jamaa na wanafamilia wake, kwa kizingizio
cha mapenzi.

Mara nyingi, wapenzi hujitenga na watu wao wa karibu kutokana na hofu na
kutokujiamini, lakini uhusiano wa aina hii hauwezi kuwa na nguvu na unaweza kujenga mazingira ya kuibuka kwa matatizo mengine ambayo hatimaye yatauua uhusiano.

5. KUTOJITAMBUA KWA MPENZI

Iwapo itatokea kuwa mmoja wa wapenzi/marafiki au wote wawili akawa hajitambui na kufuata matakwa yake, mahitaji yake, matamanio yake, mipango yake ya baadaye, malengo yake, msimamo wake, hulka yake na vipaumbele vyake, haitakuwa rahisi kwa watu hawa wawili kuwa na uhusiano wenye afya.

Kujitambua huwasaidia wapenzi kuwa huru kila mmoja kwa mwenzake, akimweleza anataka nini, jambo ambalo husaidia kuimarisha uhusiano. Lakini inapotokea kuwa mmoja wa wapenzi hajitambui, au wote wawili hawajitambui, ni rahisi sana uhusiano kuvunjika, hasa kama wahusika waliingia katika uhusiano huo wakiwa na umri mdogo.

6. KUTOJITHAMINI NA KUTOJIAMINI

Inapotokea mmoja wa wapenzi akajihisi kuwa hastahili kupendwa, hiyo inatosha kuwa sababu ya mazingira ya kuvunjika kwa uhusiano. Hali hii hutokana na kutojithamini na kutojiamini kwa mtu – mambo ambayo yanaweza kusababishwa na sababu mbalimbali yakiwamo malezi.

Kutokujiamini au kuwa na hofu ya kuachwa kunaweza kumfanya mtu ambane sana mwenzake na kumnyima uhuru – jambo ambalo halifai kwa afya na ustawi wa uhusiano. Kujiamini na kujithamini kwa mwenza ni njia mojawapo ya kuepuka kuvunjika kwa uhusiano.

7. WIVU ULIOKITHIRI

Wivu ni mojawapo ya sababu kuu za kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi au hata ndoa. Wivu wa kupindukia unaweza kusababisha ugomvi ambao nao ni sababu kubwa ya kuachana kwa wapenzi.

Wivu husababishwa zaidi na kutokujiamini kwa mtu. Kwa hiyo, ili kuepuka wivu na
kuunusuru uhusiano wa kimapenzi, lazima mtu kwanza ajithamini na kujiamini kuwa
anastahili kupendwa na mpenzi wake kama alivyo.

8. MAWASILIANO HAFIFU

Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika mapenzi. Iwapo wapenzi watashindwa kuelezana hisia zao, mawazo yao, mitazamo yao, imani zao, matatizo yao au hata furaha zao, uhusiano utakuwa unaelekea pabaya.

Inapotokea hiyo ikawa sababu ya kuachana kwa wapenzi, basi mtu anapojifunza tena
kupenda atapaswa kujifunza pia jinsi ya kuwasiliana vema na mwenzake, kwani kwa
hakika mawasiliano mabaya ni sababu kubwa ya kuachana kwa wapenzi.

9. MMOJA KUMDHIBITI MWENZAKE

Inapotokea kuwa mmoja wa wapenzi anataka kumdhibiti mwenzake na kumwendesha mithili ya mtu anayemwendesha farasi, uhusiano unaohusika utakosa mapenzi – na hiyo itakuwa sababu kubwa ya kuachana kwa wapenzi hawa baadaye.

Sababu hii inaweza kuchukuliwa katika namna tofauti. Mtu anaweza kumbana mwenzake kwa kumfuatilia muda wote, kumtishia – mathalani anapochelewa nyumbani au kwenye miadi – na kutompa ruhusa na uhuru wa kupanga ratiba zake au kutoka na watu wa karibu naye. Hii si tabia ya kimapenzi na matokeo yake ni kushindwa kwa uhusiano.

10. UNYANYASAJI

Hii ndiyo sababu ambayo pengine iko wazi zaidi. Kuna aina mbalimbali za unyanyasaji
ambao hujitokeza baina ya wapenzi na si lazima kwamba mwanamume ndiye anayemnyanyasa mwanamke kama ilivyozoeleka. Hata wanawake huwanyanyasa wanaume.

Unaweza kudhani ukinyanyaswa tu na mpenzi au mwenza utamwacha, lakini ukweli ni kwamba wengi huvumilia, pengine kutokana na kuiogopa jamii inayowazunguka. Lakini ukweli ni kwamba unyanyasaji huondoa kabisa maana ya mapenzi na kusababisha wapenzi
wengi kukosa sababu ya kuendelea kuwa pamoja.

KUWA MAKINI

Migogoro ni kitu cha kawaida katika uhusiano wa kimapenzi – na kwa hakika haiepukwi, isipokuwa wenza hujifunza jinsi ya kuimaliza na kuondoka wakiwa salama. Hata hivyo, kuna nyakati ambapo uhusiano hufikia kikomo. Una heri wewe ambaye umezifahamu sababu kuu za kuvunjika kwa uhusiano maana zitakusaidia kufahamu jinsi ya kujipanga na kutengeneza uhusiano wenye afya na mustakabali mwema.

Sunday, October 24, 2010

Tambua mpenzi anaye kudanganya/anakulaghai.

Mpenzi wako anakosa maamuzi binafsi. Hii haimaaanishi kwamba atakwenda nje kutafuta mpenzi mwingine, lakini mtu asiye na uhuru fulani katika mawazo yake mara nyingi huwa akitafuta msaada sehemu nyingine. Kama mahitaji ya mtu huyu hayatatimizwa, basi hutafuta sehemu nyingine kwa mtu mwingine ili kutimiza hisia zake.

Kila mara mpenzi wako anamlaumu mtu Fulani. Anajaribu kukufanya ufikirie kwamba aina ya watu kama hao hawamvutii kabisa, ingawa kwa hakika ndani ya nafsi yake hubakia mvuto wa siri kwa mtu wa aina hiyo. Zaidi ya yote mpenzi wako anaanza kulaumu vitu kadhaa kuhusu wewe ambavyo awali aliona vina mvutia na kumtamanisha.

Mpenzi wako anaanza tabia ya kujifungia ndani mnapokuwa pamoja, wakati hapo awali alizoea, kuuacha mlango wazi. Kwa mfano hataki muoge pamoja kama zamani, anapobadili nguo anataka usimtazame na mambo mengine kadha wa kadha.

Mpenzi wako hujiona kama mkosefu wakati unapomfanyia kitu fulani kizuri. Wewe unaonekana kuwa mtu unayefanya maisha yake kwamba mabaya na uhusiano kama kitanzi.

Kwa kufanya kitu kizuri unamlazimisha mwongo huyu kufikiria kuhusu usaliti anaokufanyia.

Mpenzi wako anaonyesha hamu ya kusoma kitabu zaidi au kuangalia televisheni kuliko kuzungumza na wewe au kufanya mapenzi na wewe.

Mpenzi wako kwa muda mrefu amekuwa mwenye mawazo lakini kila unapomuuliza hataki mjadili kuhusu mambo yake binafsi.

Mpenzi wako anaonyesha kushtuka anapoamshwa. Hali hii husababishwa na kutokuwa na uhakika ni chumba gani alicholala na yuko katika kitanda cha mpenzi gani kati ya wawili alionao.

Tabia ya mpenzi wako inawafanya rafiki zako kuanza kukuuliza nini kinachoendelea. Rafiki wa karibu na ndugu wa familia watabaini hali ya kutokuwepo na amani baina yenu wawili kabla nyie hamjaelewa sawasawa.

Tabia ya kulala kwake itabadilika, kama alikuwa akichelewa kulala, sasa anaweza kuwahi kwa kisingizio kwamba amechoka.

Anaweza kuwa kweli amechoka, lakini tabia hiyo inapoendelea ujue kuna jambo, kwani mara nyingine huwa hapendi hata kuzungumza mnapokuwa kitandani, tofauti na zamani.

Jinsi ya kupata Mpenzi wa Kweli.

Katika mahusiano yoyote yale mtu/wewe ungependa kutambua ni kwajinsi gani mpenzi wako hakudanganyi. Sasa maswali yako unaweza kujibiwa kwa kusoma mambo yafuatayo;-

Usiipe nafasi hofu Nyote mnapaswa kuwa na hisia zenye afya ili kujenga uhusiano wenye mafanikio. Kwa mfano, siyo dalili nzuri kama unakuwa kwenye uhusiano kwa sababu tu unahofu kuwa mpweke.

Ni vibaya pia kwa mwanaume wako kusema anaupenda mchezo fulani kama anavyokupenda! Au ukiwa na msongo wa mawazo, usinase kwenye mtego wa mapenzi kwa kudhani unaweza kuwa tiba. Ni vizuri zaidi kutafuta mwanaume ambaye hahitaji utabibu.

Chunga mwendo wako
Jihadhari na chunga mwenendo wako kwani wanaume huwa makini na hushangazwa zaidi wakati wapenzi wao wanapokuwa wanafanya mambo ya ajabu. Unapozungumza naye muangalie usoni siyo sakafuni.

Usimuulize maswali mengi kuhusu kazi yake, ingawa ni muhimu kujua anafanya kazi gani, kwani anaweza kuwa jambazi ati! Anaweza kudhani unataka kumchuna tu.

Kama utashindwa kuchunga tabia yako, usishangae kama kukutana kwenu siku ya kwanza kunakuwa ndio mwisho wenu na usipojiangalia utajikuta tayari umemfunulia!

Kufanana huleta mafanikio
Hii haimaanishi unapaswa kuolewa na ndugu au mzazi wako, la hasha! Lakini unapoanza uhusiano na mtu, hakikisha unamfahamu kwanza kwa undani na jiulize mara mbili kama kuna vitu ambavyo mnalingana.
Fikiria kuhusu uhangaikaji wake katika maisha (hata kama hana uwezo mkubwa kifedha, je, anajuhudi za kuzisaka hizo fedha ama la?), ujuzi na hata mapenzi ya dhati.

Na fikiria sana kama malengo katika maisha yenu yanarandana. Nyote mnapaswa kukubaliana kuhusu athari pia za ndoa na kukabiliana nazo kama kuwa na watoto, kuishi kwenye nyumba ya mbavu za mbwa au hekalu.

Vipo vitu unavyoweza kuvitambua kwa kukutana kwenu mara moja au mara mbili, na nyote mnapaswa kuwa wazi.

Toa upinzani
Mfanyie kila uwezalo mpenzi wako ili atambue kwamba unampenda, lakini usitake kuchukulia dalili zake za kuridhika na wewe mapema ndizo zikupumbaze na kumganda.

Hapa sizungumziii kanuni – usisite kuijibu simu yake atakapokupigia au kwenda kukutana naye atakapokuita, hata hivyo, epuka kukutana naye sehemu ya uficho kama chumbani, lakini usijenge maisha yako kumzunguka yeye na wala usimlazimishe akakuelezea hisia zake.

Hakikisha kwamba yeye ni nyongeza katika maisha yako na siyo muhimili wa maisha yako.

Usiwe domokaya
Najua wengi wenu mna mambo mengi ambayo mnaweza kuyazungumza, lakini yahifadhi mengine kwa ajili ya siku nyingine. Wanaume hupenda kusikia habari mpya kila mnapokutana.

Wanawake wanapaswa kufikiria kuhusu hadithi mbili au tatu kali ambazo wanaweza kuzungumza wanapokuwa kwenye miadi, lakini wasivuke mpaka na kuanza kuzungumza mambo yanayowahusu wenyewe!

Usinune
Wanaume wengi huwa wanalalamika kwamba hupata wakati mgumu zaidi wanapokuwa na wapenzi wao, hasa katika siku ya kwanza ambapo hushindwa hata kuwabusu, kama huyo uliyenaye ndiye chaguo lako, basi usiwe mgumu, tabasamu na kama atakubusu usikwepeshe uso wako.

Karibuni katika ukurasa mpya na wa aina yake!!!

Ndugu zangu napenda kuwakaribisha katika ukurasa huu wa mahusiano. Ninaposema mahusiano namaanisha mahusiano yetu sisi kama vijana, wazee, wapenzi, marafiki, wanajamii na kadhalika.

Unakaribishwa kutoa mawazo yako, maoni au ushauri wowote kuhusu mahusiano. Toa mtazamo wako kuhusu mahusiano ili tuweze kujifunza kupitia wewe.

Naanza kwa kukuuliza swali/maswali
1. Mahusiano nini?
2. Ili mahusiano yako ya KIMAPENZI yawezekudumu utatumia mbinu gani?
3. Kwanini mahusiano mengi ya KIMAPENZI yanadumu kwa kitambo kidogo na kuvunjika?