Sunday, October 24, 2010

Jinsi ya kupata Mpenzi wa Kweli.

Katika mahusiano yoyote yale mtu/wewe ungependa kutambua ni kwajinsi gani mpenzi wako hakudanganyi. Sasa maswali yako unaweza kujibiwa kwa kusoma mambo yafuatayo;-

Usiipe nafasi hofu Nyote mnapaswa kuwa na hisia zenye afya ili kujenga uhusiano wenye mafanikio. Kwa mfano, siyo dalili nzuri kama unakuwa kwenye uhusiano kwa sababu tu unahofu kuwa mpweke.

Ni vibaya pia kwa mwanaume wako kusema anaupenda mchezo fulani kama anavyokupenda! Au ukiwa na msongo wa mawazo, usinase kwenye mtego wa mapenzi kwa kudhani unaweza kuwa tiba. Ni vizuri zaidi kutafuta mwanaume ambaye hahitaji utabibu.

Chunga mwendo wako
Jihadhari na chunga mwenendo wako kwani wanaume huwa makini na hushangazwa zaidi wakati wapenzi wao wanapokuwa wanafanya mambo ya ajabu. Unapozungumza naye muangalie usoni siyo sakafuni.

Usimuulize maswali mengi kuhusu kazi yake, ingawa ni muhimu kujua anafanya kazi gani, kwani anaweza kuwa jambazi ati! Anaweza kudhani unataka kumchuna tu.

Kama utashindwa kuchunga tabia yako, usishangae kama kukutana kwenu siku ya kwanza kunakuwa ndio mwisho wenu na usipojiangalia utajikuta tayari umemfunulia!

Kufanana huleta mafanikio
Hii haimaanishi unapaswa kuolewa na ndugu au mzazi wako, la hasha! Lakini unapoanza uhusiano na mtu, hakikisha unamfahamu kwanza kwa undani na jiulize mara mbili kama kuna vitu ambavyo mnalingana.
Fikiria kuhusu uhangaikaji wake katika maisha (hata kama hana uwezo mkubwa kifedha, je, anajuhudi za kuzisaka hizo fedha ama la?), ujuzi na hata mapenzi ya dhati.

Na fikiria sana kama malengo katika maisha yenu yanarandana. Nyote mnapaswa kukubaliana kuhusu athari pia za ndoa na kukabiliana nazo kama kuwa na watoto, kuishi kwenye nyumba ya mbavu za mbwa au hekalu.

Vipo vitu unavyoweza kuvitambua kwa kukutana kwenu mara moja au mara mbili, na nyote mnapaswa kuwa wazi.

Toa upinzani
Mfanyie kila uwezalo mpenzi wako ili atambue kwamba unampenda, lakini usitake kuchukulia dalili zake za kuridhika na wewe mapema ndizo zikupumbaze na kumganda.

Hapa sizungumziii kanuni – usisite kuijibu simu yake atakapokupigia au kwenda kukutana naye atakapokuita, hata hivyo, epuka kukutana naye sehemu ya uficho kama chumbani, lakini usijenge maisha yako kumzunguka yeye na wala usimlazimishe akakuelezea hisia zake.

Hakikisha kwamba yeye ni nyongeza katika maisha yako na siyo muhimili wa maisha yako.

Usiwe domokaya
Najua wengi wenu mna mambo mengi ambayo mnaweza kuyazungumza, lakini yahifadhi mengine kwa ajili ya siku nyingine. Wanaume hupenda kusikia habari mpya kila mnapokutana.

Wanawake wanapaswa kufikiria kuhusu hadithi mbili au tatu kali ambazo wanaweza kuzungumza wanapokuwa kwenye miadi, lakini wasivuke mpaka na kuanza kuzungumza mambo yanayowahusu wenyewe!

Usinune
Wanaume wengi huwa wanalalamika kwamba hupata wakati mgumu zaidi wanapokuwa na wapenzi wao, hasa katika siku ya kwanza ambapo hushindwa hata kuwabusu, kama huyo uliyenaye ndiye chaguo lako, basi usiwe mgumu, tabasamu na kama atakubusu usikwepeshe uso wako.

No comments:

Post a Comment