Saturday, September 17, 2016

ANZISHA MAHUSIANO MAPYA WAKATI MOYO WAKO HAUNA DOWA LOLOTE

Si lazima uwe kwenye uhusiano muda wote, ukiona mambo hayajakaa vizuri usiyalazimishe.

Kabla haujaanza uhusiano mwingine, ebu JIULIZE ni kitu gani umejifunza Katika uhusiano wako uliopita.

Kuna msemo usemao KUJUA chanzo cha tatizo ni Nusu ya KUTATUA Tatizo, Je umefahamu tatizo lilofanya uhusiano wako wa 1, 2 na 3 kuvunjika? Ulishawahi kukaa chini kujiuliza? Ulipata majibu gani?

Usiingie kwenye uhusiano mpya kabla haujapona MAJERAHA ya uhusiano uliopita, Kujipa muda kuwa peke yako ni TIBA tosha.

Usiingie kwenye uhusiano mpya ili kumkomoa X wako, Isije ukajikomoa mwenyewe.

Usiingie kwenye uhusiano mpya ili kupoza moyo wako isije ukawa unazidisha Kidonda,

Usiingie kwenye uhusiano mpya ili kuondoa upweke, isije ukauzidisha huo upweke.

Usiingie kwenye uhusiano mpya ukitegemea kumpata mtu BORA kuliko X wako, isije ukawa unaruka Mkojo, unakanyaga.........?

Usiwe kama Nyani kuruka-ruka kwenye miti, mara tawi hili, mara tawi lile. Lakin pamoja na uhodari wote wa Nyani wa kuruka kwenye miti lakini kama siku ya KUFA imefika, miti yote HUTELEZA.

SI LAZIMA MUDA WOTE UWE KWENYE UHUSIANO, JIPE MUDA KUWA PEKE YAKO, CHUKUA LIKIZO YA MAPENZI.

"MOYO ULIOJERUHIWA, HUJERUHI, MOYO ULIOPENDWA HUPENDA "